Eng. Peter Ulanga

CEO & Fund Manager: UCSAF

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Katika kuadhimisha WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, 2017 itakayoanza tarehe 16 na kumalizika tarehe 23 Juni, MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE unapenda  kuwataarifu wadau wa  huduma za mawasiliano hususani katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yasiyo na mvuto kibiashara na wananchi kwa ujumla kuwa MFUKO umetenga siku mbili mahususi kwa ajili ya kupokea na kuyatolea ufafanuzi malalamiko na kero kutoka kwa wananchi, kuhusu huduma za mawasiliano hususani katika maeneo ya vijijini. Zoezi hilo la kukutana na wadau litafanyika kati ya tarehe 21 na 22 Juni 2017, kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni, katika ofisi za MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE zilizoko katika ghorofa ya pili ya Jengo la TTCL Kijitonyama ,  Jijini Dar es Salaam. Aidha, kwa wadau watakaoshindwa kufika katika ofisi za MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE, bado wanayo nafasi ya kuwasilisha kero, dukuduku, maoni au malalamiko yao kupitia simu namba +255 22 2700000 au kwa njia ya barua pepe: ceo@ucsaf.go.tz. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika Utoaji Huduma,Vijana washirikishwe kuleta mabadiliko Barani Afrika".

Habari na Matukio
WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Tarehe : 2017-06-21

Katika kuadhimisha WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, 2017 itakayoanza tarehe 16 na kumalizika tarehe 23 Juni, MFUKO WA MAWASIL ...

Zaidi
UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE
Tarehe : 2016-09-07

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi an Mawasiliano Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa (Mb) kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu ...

Zaidi
Girls in ICT Day - Tanzania
Tarehe : 2016-04-06

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeandaa warsha ya uvumbuzi wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa ...

Zaidi