Eng. Peter Ulanga

CEO & Fund Manager: UCSAF

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi an Mawasiliano Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa (Mb) kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu 7(3) cha Sheria ya Huduma za Mawasiliano kwa Wote Namba 11 ya mwaka 2006 amemteua Dkt. Joseph S.Kilongola kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 16/8/ 2016.

Dkt. Joseph S. Kilongola ni mhandisi aliyebobea katika mawasiliano na ubunifu wa mifumo aliyewahi kutumikia nafasi mbalimbali katika Kampuni ya Simu Tanzania na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Hadi kustaafu kwake Dkt. Joseph S Kilongola alikuwa Mkurugenzi wa TEHAMA katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Dkt. Joseph S. Kilongola alihitimu shahada ya uzamivu katika mawasiliano na ubunifu wa mifumo na shahada ya uzamili katika sayansi ya mipango ya mifumo, teknolojia ya habari na uchumi wa viwanda zote kutoka Chuo Kikuu cha usafirishaji na mawasiliano cha Dresden, Ujerumani.

Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na wafanyakazi wote wa Mfuko tunapenda kutoa pongezi zetu za dhati kwa Dkt. Joseph S.Kilongola kwa uteuzi huo na kuamini kuwa uzoefu wake mkubwa katika sekta ya mawasiliano utafanikisha kufikia malengo na dira ya Mfuko.

 

Imetolewa na

Mtendaji Mkuu

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote

 

Habari na Matukio
WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Tarehe : 2017-06-21

Katika kuadhimisha WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, 2017 itakayoanza tarehe 16 na kumalizika tarehe 23 Juni, MFUKO WA MAWASIL ...

Zaidi
UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE
Tarehe : 2016-09-07

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi an Mawasiliano Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa (Mb) kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu ...

Zaidi
Girls in ICT Day - Tanzania
Tarehe : 2016-04-06

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeandaa warsha ya uvumbuzi wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa ...

Zaidi